Baba amezini na msichana wake baada ya kulewa

Swali: Ni ipi hukumu ya mwanaume anayezini na msichana wake ilihali amelewa?

Jibu: Anatakiwa kuadhibiwa. Kuhusu kusimamishiwa adhabu kwa mujibu wa Shari´ah hapana. Hana adhabu kwa mujibu wa Shari´ah ikiwa amelewa kutokana na maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amenisamehe ummah wangu kwa ajili yangu makosa, usahaulifu na yale wanayotenzwa nguvu kwayo.”

“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu aina tatu; aliyelala mpaka anapoamka, mtoto mpaka anapobaleghe na mwendawazimu mpaka anapopata akili.”[1]

Miongoni mwao akataja mwendawazimu mpaka apate tena akili. Huyu yuko katika hukumu ya wendawazimu. Bakora ziwe za wastani; isiwe kubwa kiasi cha kwamba ukavunja mfupa, na usiwe mdogo kiasi cha kwamba hauumizi. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَائِفَةٌ مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ

”Washuhudie adhabu yao kundi la waumini.”[2]

Anatakiwa kupigwa kipigo cha wastani. Asipigwe kwa nguvu sana. Muhimu aadhibiwe.

[1] Abu Daawuud (4405) na Ahmad (1362). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2/5).

[2] 24:02

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 256
  • Imechapishwa: 02/04/2025