Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy ana sifa maalum zifuatazo:

1- Ana mapenzi ya nguvu juu ya Sunnah.

2- Ni mwenye kutilia umuhimu ´Aqiydah.

3- Ana uelewa mzuri wakati anapofanya hitimisho.

4- Ana chuki yenye nguvu kabisa juu ya u-Hizbiyyah iliyowafarikisha wailsamu.

5- Anapopambaukiwa na haki anashikamana nayo kweli kweli na hajali anayeonelea kinyume yeyote awae.

6- Ana mapenzi makubwa kwa Ahl-us-Sunnah na kuwachukia watu wa Bid´ah.

7- Ana unyenyekevu, urafiki, upole na umakinifu. Allaah amemtunukia neema hii mpaka wanafunzi na watu wa kawaida wakawa wanampenda.

Ninamuomba Allaah Mkubwa atufanye sisi na yeye kuunufaisha Uislamu na waislamu. Hakika Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.

Imeandikwa na:

Abu ´Abdir-Rahmaan Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Utangulizi wa “al-Qawl al-Mufiyd fiy Adillat-it-Tawhiyd”, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 27/08/2020