Swali: Hadiyth inasema:
”Aliswali (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bila kuelekea ukutani.”
Kama alivyoeleza mfafanuzi…
Jibu: Huenda ilikuwa kuielekea Sutrah nyingine. Si lazima iwe hivo. Haimaanishi kwa yakini kwamba hakuwa na Sutrah. Huenda alikuwa na Sutrah aina ya mkuki au mfano wake.
Swali: Haafidhw ametaja upokezi wa al-Bazzaar kwamba alikuwa akiswali bila kitu chochote kinachomkinga?
Jibu: Inawezekana, kwa kuwa alifanya hivyo alipomtembelea ‘Abbaas sehemu yake. Hivyo ikafahamisha kwamba Sutrah siyo wajibu. Ni Sunnah tu, siyo jambo la lazima. Kwa hiyo kilichotokea ni kwamba mtu alipita mbele ya sehemu ya safu ya waumini. Kupita mbele ya safu hakubatilishi swalah, hata ikiwa imamu hana Sutrah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27563/هل-صح-حديث-في-الصلاة-الى-غير-سترة
- Imechapishwa: 06/04/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)