Baada ya ndoa mume amegundua kuwa mkewe alikuwa akifanya mabalaa

Swali: Mwenye kuoa mke kisha baada ya ndoa mwanamke akatubia na yeye mwanaume hajui kuwa ya nyuma aliyoyafanya mwanamke yalikuwa mabaya.

Jibu: Hapana vibaya akiwa ni mwanamke wa Kiislamu. Akiwa ni mwanamke wa Kiislamu ambaye alikuwa na maasi kisha baadaye akatubia himdi zote njema anastahiki Allaah. Lakini kama alikuwa mwanamke kafiri haijuzu kwa mwanaume wa Kiislamu kumuoa mwanamke kafiri – kama vile mwabudia mizimu – muda wa kuwa sio myahudi au mnaswara.  Lakini ni sawa kumuoa akiwa ni mwanamke wa kiyahudi au mnaswara anayejilinda na machafu.

Swali: Ni mwanamke wa Kiislamu lakini mume amejua baadaye kwamba alikuwa anazini?

Jibu: Ndoa ni sahihi muda wa kuwa uinje wake ni ameshatubia na ni mwema.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23908/ما-يفعل-من-علم-بسوء-تابت-منه-زوجته
  • Imechapishwa: 30/05/2024