Swali: Nimenunua ardhi kwa kiasi cha 1,100,000 SAR na imebaki kwangu kwa muda wa miaka minane na sasa nimeiuza kwa kiasi cha 5,000 SAR. Je, nitoe zakaah ya kiasi cha awali kwa muda wa miaka minane au kiasi cha sasa ambacho ni 50,000 SAR kwa mwaka mmoja au kwa miaka minane?

Jibu: Iwapo ardhi uliikusudia kwa ajili ya biashara na nia yako ni kuuza, basi unatoa zakaah yake kila mwaka kwa kile inachostahili kila mwaka kulingana na thamani yake kwa watu wa maarifa, inaweza kukadiriwa kuwa 1,000, 2,000 au 3,000 kwa mujibu wa wanavyosema wataalamu wa ardhi zinazofanana nayo na zinazokaribiana nayo. Kila mwaka una hesabu yake na una kiwango chake. Mwaka wa mwisho unatoa zakaah ya 5,000. Ama kutoa zakaah kwa miaka yote kwa jumla, hapana. Kila mwaka una hukumu yake na una thamani yake iwapo ulikuwa umeikusudia biashara. Iwapo uliinunua bila kuwa na nia ya biashara, ulikuwa una shaka je, utaiuza au utaijenga au utafanya nini. Kwa maana nyingine hukuwa na uamuzi wa yakini, basi hakuna zakaah juu yako. Lakini kama ulikuwa umeazimia kwa yakini kwamba umeishikilia kwa ajili ya biashara, unataka kuiuza na kufanya biashara nayo, basi ni wajibu juu yako kutoa zakaah kila mwaka kwa thamani ya ardhi hiyo. Ni mamoja iwe ni ya bei ndogo au ya bei kubwa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2379/حكم-زكاة-العقار-عند-بيعه
  • Imechapishwa: 10/07/2026