Swali: Muulizaji anauliza kuhusu fedha anazochangia katika ardhi. Je, zinawajibikiwa na zakaah?

Jibu: Ikiwa ardhi hiyo imeandaliwa kwa ajili ya biashara, basi atatoa zakaah ya sehemu yake katika ardhi hiyo baada ya kuangalia thamani yake. Anaweza kuikadiria yeye pamoja na baadhi ya ndugu zake wanaoifahamu thamani ya ardhi hiyo. Ikiwa dhana yenye nguvu itampelekea kwamba thamani yake ni kadhaa fulani, basi atatoa zakaah.

Swali: Vipi kama hakutoa ila 5,000 tu?

Jibu: Hilo linategemea hali yake, atatoa zakaah ya sehemu yake katika ardhi hiyo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1424/كيفية-زكاة-الارض-المعدة-للتجارة
  • Imechapishwa: 25/12/2025