ar-Raajihiy kucheza mpira na kaptula na kuwatazama wenye hali hiyo

Swali: Ni ipi hukumu ya kucheza mpira kwa kaptula fupi inayoonyesha mapaja? Je, inajuzu kucheza na mfano wa watu kama hawa? Inajuzu kwa wale walioshiriki kucheza na mfano wa kaptula kama hizi?

Jibu: Ikiwa haifichi kutokea kwenye kitovu mpaka kwenye magoti haijuzu. Maoni ya sawa ni kwamba kutokea kwenye kitovu mpaka kwenye magoti ni viungo visivyotakiwa kuonekana. Kuna Hadiyth nyingi zimekuja kuhusu hilo. Ni wajibu kwake kujisitiri kwa suruwali pana isiyoonyesha kitu na wala ambayo mtu hawezi nyuma yake kuona rangi ya ngozi kama ni nyekundu, nyeusi au nyeupe. Vilevile haitakiwi kuwa ya kubana kwa kiasi cha kwamba inaonyesha fomu ya mwili. Bali inatakiwa iwe suruwali pana na inayoficha kuanzia kwenye kitovu mpaka kwenye magoti.

Ikiwa anaswali na kaptula fupi inayoonyesha mapaja basi swalah haisihi. Haijuzu kwa mtu kumtazama wala kucheza naye.  Kwa sababu huyu anavuka mipaka ya Allaah. Maandiko yamefahamisha kwamba ni wajibu kwa mtu kusitiri viungo vyake visivyotakiwa kuonekana Kishari´ah kuanzia katika kitovu mpaka kwenye mapaja. Kama ilivyokuja katika Hadiyth:

“Mapaja ni ´Awrah.”

“Usitazame mapaja ya aliyehai wala ya maiti.”

Japokuwa imezungumziwa, lakini hata hivyo ina mapokezi yenye kuitolea ushahidi.

Kinacholengwa ni kwamba mapaja ni kiungo kisichotakiwa kuonekana kwa mujibu wa maoni sahihi ya wanachuoni wahakiki. Haijuzu kwa mtu kuonyesha kitu katika mapaja ndani ya swalah, katika michezo, sehemu nyingine wala kuwatazama.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 27/09/2018