ar-Raajihiy bora kati ya Tahliyl na Istighfaar

Swali: Ni lipi bora zaidi; kusema “Subhaan Allaah”, “Laa ilaaha illa Allaah” au “Astaghfiru Allaah”?

Jibu: Kusema “Subhaan Allaah”, “Laa ilaaha illa Allaah” ndio bora zaidi. Kwa sababu ni ´ibaadah na ni kumsifu Allaah. Kusema “Astaghfiru Allaah” ni du´aa na ni kuomba msamaha. Yote ni ´ibaadah na kheri. Lakini Tasbiyh ndani yake kuna kumsifu Allaah (´Azza wa Jall). Muumini anatakiwa kukusanya baina ya haya na haya. Mara anatakiwa kusema “Subhaan Allaah”, mara aseme “Laa ilaaha illa Allaah”. Anatakiwa kusema “Subhaan Allaah”, “Laa ilaaha illa Allaah”, “Allaahu Akbar” na kumuomba Allaah. Yote ni kumwabudu Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (09) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191370#219699
  • Imechapishwa: 16/03/2019