Swali: Sauti haiko wazi na tumechoweza kusikia tu ni kama inajuzu kufanya filamu ya Mitume…

Jibu: Haijuzu kufanya filamu ya Mitume. Haijuzu kufanya filamu ya Mitume wala kuwachora. Bali haijuzu hata kuwaigiza Maswahabah. Huku ni kuwatukana. Ikiwa makusudio ni kutaka kueneza Da´wah yao, unaweza kubainisha Da´wah yao kwa bayana na maneno na uandishi. Ama kuhusu kuchora sura zao haijuzu. Ni haramu na ni kuwatukana. Hata kuchora sura za Maswahabah haijuzu. Ikiwa kuwachora Maswahabah haijuzu tusemeje kuhusu Mitume? Huku ni kuwatukana. Kitendo hichi kinaweza kupelekea katika kuritadi na tunamuomba kinga Allaah. Lakini hata hivo pengine mtu huyu hakukusudia kuwatukana. Kwa hali yoyote kuwachora ni kuwatukana. Hivyo, haijuzu kuwachora wala kuwaigiza. Zitajwe fadhila zao na ulinganizi wao na wema wao kwa ubainifu, mawaidha, Khutbah na uandishi pasina kuwa na haja ya kufanya picha zao na kuwachora.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4738
  • Imechapishwa: 01/05/2015