Swali: Vipi ikiwa mtu anaomba lakini kwa ajili ya ulingano kama vile ujenzi wa misikiti n.k.?

Jibu: Huu ni uombezi kwa watu wema ambao unawalingania kufanya wema. Awaombee wale wanaoimarisha msikiti, wanaonunua vitabu vya kuwagawia wanafunzi au kwa ajili ya kujenga masomo ya dini. Haya yanaingia katika maneno Yake:

مَّن يَشْفَعْ شَفَاعَةً حَسَنَةً يَكُن لَّهُ نَصِيبٌ مِّنْهَا

“Atakayeombea uombezi mzuri atapata fungu lake katika hayo.”[1]

[1] 04:85

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28828/حكم-من-يسال-المال-من-اجل-الدعوة-والمساجد
  • Imechapishwa: 18/05/2025