Swali: Ni ipi hukumu ya kusema kila ambaye anatetea msingi wa kusikiliza na kumtii kiongozi ni Murjiy´?

Jibu: Achana nao. Ni maneno ya kipuuzi. Sisi tunawatetea watawala wa waislamu kwa sapoti ya Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Qur-aan. Watawala wa waislamu wana utukufu na nafasi yao. Haijuzu kuwaponda. Mtu kama huyu anadhoofisha mkusanyiko, analeta uadui kati ya watawala na wananchi na husababisha shari kubwa. Haijuzu kabisa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/msrf–16041434.mp3
  • Imechapishwa: 24/09/2020