Anayemtaja Allaah na moyo uliyoghafilika

Swali: Je, mtu anapata thawabu ikiwa anamtaja Allaah huku moyo wake umeghafilika?

Jibu: Inategemea hali yake. Kila mtu anapata fungu lake. Moyo wa mtu ukikusanyika, basi jambo linakuwa kamili. Ikiwa ni moyo peke yake, anapata fungu lake. Ikiwa ulimi peke yake, ana fungu lake. Lakini vikikusanyika vyote vitatu – moyo, ulimi na viungo – huo ndio ukamilifu.

Swali: Vipi kuhusu thawabu zinazopelekea?

Jibu: Kila mtu hupata thawabu kulingana na kuhudhuria moyo wake na kulingana na matendo yake.

Swali: Mtu anayefanya Adhkaar za asubuhi na jioni huku moyo wake umeghafilika zinamfaa?

Jibu: Ndiyo, lakini thawabu yake inakuwa kulingana na kiwango cha kuhudhurika kwa moyo wake. Kadiri anavyozidi kuwa na moyo uliohudhuria, ndivyo thawabu yake inavyokuwa kubwa zaidi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31172/هل-يحصل-الاجر-لمن-ذكر-الله-وقلبه-لاه
  • Imechapishwa: 10/10/2025