Anayegusa tupu au uke wake baada ya wudhuu´ kabla ya josho la janaba

Swali: Je, mtu aanze kutawadha kabla ya kuanza kuoga na wakati mwingine anaweza kugusa tupu yake wakati wa kujisafisha?

Jibu: Hatakiwi kugusa tupu yake. Akishatamba kwa maji na akaoga kwa nia ya twahara, basi amemaliza. Lakini kama ataosha sehemu za kando yake na akagusa kwa mkono wake maeneo ya karibu nayo, haidhuru.

Swali: Kwa hiyo unakusudia kwamba kabla ya kuanza kuoga aanze kutawadha?

Jibu: Ndio, kisha atawadhe wudhuu´ wa swalah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24753/حكم-مس-الفرج-بعد-الوضوء-وقبل-الغسل
  • Imechapishwa: 06/12/2024