Swali: Ikiwa niko juu ya mojawapo ya madhehebu, kama madhehebu ya Hanbaliy kwa mfano, je, ni juu yangu kuchukua ruhusa kutoka katika madhehebu mengine?
Jibu: Juu yako ni kufuata dalili, si kufuata ruhusa. Baadhi ya Salaf wamesema:
”Yule anayefuatafuata ruhusa basi huwa zandaki.”
Kila madhehebu hupatikana ndani yake makosa fulani aidha kutoka kwa baadhi ya wafuasi wake au kutoka kwa imamu anayehusishwa nayo, kwa kuwa huenda alikosea katika baadhi ya mapokezi au zikamfichikia baadhi ya Hadiyth. Hivyo mwanafunzi hapaswi kufuatilia ruhusa. Ikiwa katika suala kuna maoni tofauti na si suala la maafikiano, basi yapo maandishi na maelezo ya wanazuoni. Mwanafunzi anatakiwa achunguze dalili na aangalie maoni yaliyo karibu zaidi na yaliyo na nguvu zaidi kwa mujibu wa dalili, kisha achukue yale yaliyosimama juu ya dalili, si kufuatilia ruhusa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2138/حكم-تتبع-رخص-الفقهاء
- Imechapishwa: 02/01/2026
Swali: Ikiwa niko juu ya mojawapo ya madhehebu, kama madhehebu ya Hanbaliy kwa mfano, je, ni juu yangu kuchukua ruhusa kutoka katika madhehebu mengine?
Jibu: Juu yako ni kufuata dalili, si kufuata ruhusa. Baadhi ya Salaf wamesema:
”Yule anayefuatafuata ruhusa basi huwa zandaki.”
Kila madhehebu hupatikana ndani yake makosa fulani aidha kutoka kwa baadhi ya wafuasi wake au kutoka kwa imamu anayehusishwa nayo, kwa kuwa huenda alikosea katika baadhi ya mapokezi au zikamfichikia baadhi ya Hadiyth. Hivyo mwanafunzi hapaswi kufuatilia ruhusa. Ikiwa katika suala kuna maoni tofauti na si suala la maafikiano, basi yapo maandishi na maelezo ya wanazuoni. Mwanafunzi anatakiwa achunguze dalili na aangalie maoni yaliyo karibu zaidi na yaliyo na nguvu zaidi kwa mujibu wa dalili, kisha achukue yale yaliyosimama juu ya dalili, si kufuatilia ruhusa.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2138/حكم-تتبع-رخص-الفقهاء
Imechapishwa: 02/01/2026
https://firqatunnajia.com/anayefuata-ruhusa-za-wanazuoni-huwa-zandiki/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket