Anayeficha ushahidi kwa kukhofia juu ya nafsi yake

Swali: Anayeficha ushahidi kwa kuchelea juu ya nafsi yake?

Jibu: Allaah anasema:

تَكْتُمُوا الشَّهَادَةَ ۚ وَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ

”Msifiche ushahidi; na mwenye kuuficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi.”[1]

Ni lazima kwake kutekeleza ushahidi. Hata hivyo ikiwa hali inapelekea kwamba anaogopa kuuliwa anapewa udhuru. Lakini ahakikishe – kwa kiasi cha inavowezekana – kuutimiza kwa njia yoyote. Ingawa kwa njia ambayo haitotambulika kuwa si yeye ndiye ametoa ushahidi huo. Hakimu anaweza kusema:

“Nimepewa ushahidi na watu waadilifu au nimepewa ushahidi hivi.”

Ikiwa hakimu anaweza kufanya hivo.

[1] 02:283

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23927/ما-حكم-من-كتم-الشهادة-خوفا-على-نفسه
  • Imechapishwa: 01/06/2024