Anayefanya matendo kwa ajili ya dunia

Swali: Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Ameangamia mja wa dinari.”

Je, hapa ameingia ndani ya shirki?

Jibu: Anayefanya kazi kwa ajili ya dinari huwa ameingia katika shirki ndogo, ikiwa amefanya matendo yake kwa ajili ya dunia. Lakini ikiwa hana imani wala uchaji Allaah, basi hiyo huwa ni shirki kubwa. Lakini ikiwa amefundisha, kuamrisha au kukataza kwa ajili ya dunia, si kwa ajili ya Allaah, basi hiyo ni katika aina ya shirki ndogo:

”Ameangamia mja wa dinari.”

Ama ikiwa anafanya kwa ajili ya Allaah lakini akapewa chochote kinachomsaidia, basi hakuna tatizo. Inafaa kupewa riziki inayomsaidia katika hilo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31130/ما-حكم-من-جاء-فيه-تعس-عبد-الدينار
  • Imechapishwa: 04/10/2025