Swali: Baadhi ya watu wanajitetea kwa kusema kwamba ikiwa sitauza sigara, basi hawatanunua kutoka kwangu. Je, una mwongozo wowote kwao?
Jibu: Huo sio udhuru unaokubalika katika Shari´ah. Hili ni kama mfano wa mtu anayesema ”Nisipoweka sigara, basi hakuna mtu atakayekuja kwangu.” Hiki si kisingizio. Ni lazima amche Allaah na ajihadhari na yale aliyoharamisha Allaah, haijalishi kitu hata kama hakujiliwa na yeyote. Kile ambacho ameandikiwa na Allaah kitamjilia. Aweke bidhaa ambazo watu watafaidika nazo, ni mamoja atajiwa na watu au hapana. Hakuna haja ya kuweka kitu cha haramu. Hii ni kutokana na uchochezi na ghiliba za shaytwaan.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29349/حكم-من-يبرر-بيعه-الدخان-بحاجته-للزباىن
- Imechapishwa: 02/06/2025
Swali: Baadhi ya watu wanajitetea kwa kusema kwamba ikiwa sitauza sigara, basi hawatanunua kutoka kwangu. Je, una mwongozo wowote kwao?
Jibu: Huo sio udhuru unaokubalika katika Shari´ah. Hili ni kama mfano wa mtu anayesema ”Nisipoweka sigara, basi hakuna mtu atakayekuja kwangu.” Hiki si kisingizio. Ni lazima amche Allaah na ajihadhari na yale aliyoharamisha Allaah, haijalishi kitu hata kama hakujiliwa na yeyote. Kile ambacho ameandikiwa na Allaah kitamjilia. Aweke bidhaa ambazo watu watafaidika nazo, ni mamoja atajiwa na watu au hapana. Hakuna haja ya kuweka kitu cha haramu. Hii ni kutokana na uchochezi na ghiliba za shaytwaan.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29349/حكم-من-يبرر-بيعه-الدخان-بحاجته-للزباىن
Imechapishwa: 02/06/2025
https://firqatunnajia.com/anauza-sigara-kwa-hoja-ya-wateja-wasikimbie/