Swali: Mtazamo wa mwenye kuswali unatakiwa uwe wapi ndani ya swalah?

Jibu: Sunnah ni kwamba atazame mahali pa kusujudia wakati wa kusimama, na pia wakati wa kurukuu kwake. Ama katika hali ya kuketi chini, aangalie mahali anapoashiria kwa kidole chake anapokaa kwa ajili ya Tashahhud au kati ya sijda mbili, aangalie mahali pa ishara, kama ilivyokuja katika Sunnah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/244)
  • Imechapishwa: 02/03/2026