Swali: Katika kutubu ni lazima kuomba msamaha kwa mwenye haki juu ya anayetubu. Je, hili linamlazimisha mtu awaambie wazazi wa msichana kwamba amezini naye ili awaombe msamaha na radhi?
Jibu: Hapana. Hili linahusu pale mtu anapokuwa amechukua mali ya watu, amemuua mtu, amempiga na mfano wa hayo, hapo ndipo panapohitajika kuomba msamaha kwa mwenye haki. Ama maasia ya uzinifu – Allaah atuepushe – hili linahitaji tawbah baina ya mja na Mola wake tu. Kila mmoja hutubu kati yake na Allaah na wala hasambazi jambo hilo. Tawbah katika jambo hili ni baina yake na Allaah. Anatubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), anamwomba msamaha, anajuta kwa majuto makubwa, anaacha kabisa dhambi hiyo na anaazimia kwa dhati kutorudia tena. Mwanamke pia anatubu hivyo hivyo. Anayetubu, basi Allaah humkubalia tawbah yake. Si sharti kuwaambia familia yake juu ya jambo hilo, hapana.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1738/حكم-استسماح-الزاني-من-اهل-الفتاة-عند-توبته
- Imechapishwa: 27/12/2025
Swali: Katika kutubu ni lazima kuomba msamaha kwa mwenye haki juu ya anayetubu. Je, hili linamlazimisha mtu awaambie wazazi wa msichana kwamba amezini naye ili awaombe msamaha na radhi?
Jibu: Hapana. Hili linahusu pale mtu anapokuwa amechukua mali ya watu, amemuua mtu, amempiga na mfano wa hayo, hapo ndipo panapohitajika kuomba msamaha kwa mwenye haki. Ama maasia ya uzinifu – Allaah atuepushe – hili linahitaji tawbah baina ya mja na Mola wake tu. Kila mmoja hutubu kati yake na Allaah na wala hasambazi jambo hilo. Tawbah katika jambo hili ni baina yake na Allaah. Anatubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), anamwomba msamaha, anajuta kwa majuto makubwa, anaacha kabisa dhambi hiyo na anaazimia kwa dhati kutorudia tena. Mwanamke pia anatubu hivyo hivyo. Anayetubu, basi Allaah humkubalia tawbah yake. Si sharti kuwaambia familia yake juu ya jambo hilo, hapana.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1738/حكم-استسماح-الزاني-من-اهل-الفتاة-عند-توبته
Imechapishwa: 27/12/2025
https://firqatunnajia.com/anataka-kuwaomba-msamaha-wa-uzinzi-familia-ya-msichana/