Anataka kuanza I´tikaaf Maghrib ya tarehe 20

Swali: Je, ni bora kwa mtu anayetaka kukaa I´tikaaf kuingia baada ya Magharib siku ya tarehe 20 ili aweze kuhuisha usiku?

Jibu: Hakuna tatizo na hakuna kizuizi. Lakini Sunnah ni kuingia baada ya swalah ya Fajr, kwa ajili ya kumwigiliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25440/ما-السنة-في-وقت-بدء-الاعتكاف
  • Imechapishwa: 20/03/2025