Swali: Vipi tunawaraddi wale wanaosema kuwa wewe na wanafunzi wako mna msimamo mkali?

Jibu: Nadhani kuwa hakuna anayesema hivo isipokuwa tu mwanachama anayetoka katika taasisi ya al-Hikmah. Anayesema hivo kuwa msimamo mkali hajaujua Uislamu. Kuna haramu ipi tumeifanya kuwa ni halali ili tuzingatiwe kuwa tuna msimamo mkali? Kuna halali ipi tumeifanya kuwa ni haramu ili tuzingatiwe kuwa tuna msimamo mkali? Kuna jambo lipi lililopendekezwa tumelifanya kuwa ni wajibu ili tuzingatiwe kuwa tuna msimamo mkali? Bali ukweli wa mambo ni kwamba sisi tunachukulia wepesi. Hatuna msimamo mkali. Natamani laiti tungelikuwa wakati na kati.

Je, tuna msimamo mkali tunaposema kuwa kunyoa ndevu ni haramu na kujengea hoja kwa Hadiyth inayosema:

“Punguzeni masharubu na fugeni ndevu.”[1]?

Je, tuna msimamo mkali tunapochukia mirungi?

Je, tuna msimamo mkali tunapochukia uvutaji sigara?

Je, tuna msimamo mkali tunapochukia uigizaji?

Je, tuna msimamo mkali tukiona kuwa uchukuaji picha ni haramu?

Je, tuna msimamo mkali vyamavyama hivi vinawatenganisha waislamu?

[1] al-Bukhaariy, Muslim, Abu ´Awaanah na al-Bayhaqiy kupitia kwa Naafiy´.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 344-345
  • Imechapishwa: 10/05/2025