Swali: Ni ipi hukumu ya masuluhisho yanayofanyika baina ya koo, ikiwa wapo wanaume wawili waliotumbukia katika Shighaar[1], kisha ukajaribu kuwaficha na kuwaweka mbali na ukawasuluhisha ili wasiendelee na Shighaar baina yao? Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Hili si suluhu, maana yake ni kuondoa Shighaar. Wakiwa wameoana kwa Shighaar hilo halijuzu. Ni wajibu kwa kila mmoja wao kubadilisha ndoa ile kwa ndoa ya Kishari´ah. Ikiwa mtu atasababisha kwa kuwaelekeza na kuwafundisha mpaka wabadili ndoa batili kwa ndoa ya Kishari´ah, basi Allaah amlipe kheri.
Swali: Hapana hawakubadili, wameendelea na ile ada yao ya zamani?
Jibu: Hapana, huyo amewasaidia katika batili na anakuwa dhalimu. Huyo amewasaidia katika batili. Ama anayewasaidia katika kheri na kuwashauri na kuwaambia wabadilishe, muoe kwa mkataba wa Kishari´ah bila masharti ya mwanamke wa pili, au kama hataki akuache, basi huyo ndiye aliyefanya wema. Lakini akiwa anasema waache mambo yao, hakuna kilichotokea, waendelee tu na batili, basi huko ni kusaidiana katika dhambi na uadui.
[1] Shighaar maana yake ni mwanamume kumuoza ndugu yake wa kike kwa mwanamume mwingine, kwa sharti kwamba mwanamume huyu mwingine naye amuoze ndugu yake wa kike bila mahari yoyote kutoka kwa yeyote kati ya wanawake wawili hao (www.almaany.com)
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1002/حكم-من-ساعد-في-استمرار-نكاح-الشغار
- Imechapishwa: 31/12/2025
Swali: Ni ipi hukumu ya masuluhisho yanayofanyika baina ya koo, ikiwa wapo wanaume wawili waliotumbukia katika Shighaar[1], kisha ukajaribu kuwaficha na kuwaweka mbali na ukawasuluhisha ili wasiendelee na Shighaar baina yao? Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Hili si suluhu, maana yake ni kuondoa Shighaar. Wakiwa wameoana kwa Shighaar hilo halijuzu. Ni wajibu kwa kila mmoja wao kubadilisha ndoa ile kwa ndoa ya Kishari´ah. Ikiwa mtu atasababisha kwa kuwaelekeza na kuwafundisha mpaka wabadili ndoa batili kwa ndoa ya Kishari´ah, basi Allaah amlipe kheri.
Swali: Hapana hawakubadili, wameendelea na ile ada yao ya zamani?
Jibu: Hapana, huyo amewasaidia katika batili na anakuwa dhalimu. Huyo amewasaidia katika batili. Ama anayewasaidia katika kheri na kuwashauri na kuwaambia wabadilishe, muoe kwa mkataba wa Kishari´ah bila masharti ya mwanamke wa pili, au kama hataki akuache, basi huyo ndiye aliyefanya wema. Lakini akiwa anasema waache mambo yao, hakuna kilichotokea, waendelee tu na batili, basi huko ni kusaidiana katika dhambi na uadui.
[1] Shighaar maana yake ni mwanamume kumuoza ndugu yake wa kike kwa mwanamume mwingine, kwa sharti kwamba mwanamume huyu mwingine naye amuoze ndugu yake wa kike bila mahari yoyote kutoka kwa yeyote kati ya wanawake wawili hao (www.almaany.com)
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1002/حكم-من-ساعد-في-استمرار-نكاح-الشغار
Imechapishwa: 31/12/2025
https://firqatunnajia.com/anasaidia-kuendeleza-ndoa-ya-shighaar/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket