Anapokuomba nduguyo kumfanyia matabano

Swali: Vipi mtu akiombwa kumfanyia matabano mwingine?

Jibu: Yeye ndiye anajijua zaidi. Akimuomba yeye ndiye anajijua zaidi. Mwombwaji ana khiyari; akitaka ataitikia na akitaka ataacha. Mwombwaji ana khiyari; akiitikia ni sawa na akiacha ni sawa. Jambo ni lenye wasaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kufanya matabano kutokana na kijicho na homa. Kwa hivyo hilo likafahamisha kwamba imesuniwa kwa mwombwaji kuitikia ili aweze kumnufaisha ndugu yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24373/ما-الحكم-اذا-سىل-الانسان-ان-يرقي-غيره
  • Imechapishwa: 03/10/2024