Swali: Vipi kuhusu ambaye amekufa kwa kuchomeka na moto?

Jibu: Huoshwa ikiwa inawezekana, na kama haiwezekani atafanyiwa Tayammum. Ikiwa wanaweza kumuosha aliyeunguzwa, ni sawa. Lakini kama kuosha kutasababisha maji kuondoa baadhi ya viungo vyake kwa sababu ya kuungua, basi atafanyiwa Tayammum. Hata hivyo ikiwa jambo la kumosha ni rahisi na kuungua kwake hakuzuii kumuosha, hapana vibaya. Lakini ikiwa moto umemkata na kumchoma kiasi cha kumzuia kuoshwa, basi atafanyiwa Tayammum.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31528/هل-يغسل-من-مات-حريقا
  • Imechapishwa: 31/10/2025