Anaona haya kutoka kwenye safu baada ya kuchenguka wudhuu´ wake

Swali: Mtu aliingia ndani ya swalah akiwa katika safu ya kwanza, kisha akapatwa na hadathi lakini akaendelea na swalah ili asiikate na kulazimika kupita katika safu za nyuma na kuzivuruga na kupoteza unyenyekevu wa wanaoswali. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Tunatarajia Allaah amsamehe. Lakini lililo wajibu ni kwamba mtu akipata hadathi akiwa katika swalah au akakumbuka kuwa hana twahara, basi aikate swalah yake na aende kutawadha, kisha arudi na kuswali kile atachokiwahi katika swalah ya mkusanyiko.

Ama safu za maamuma, basi Sutrah ya imamu ndio Sutrah yao. Hivyo akipita mbele ya maamuma hapana vibaya. Aidha ni wajibu juu yake wakati wa kutoka katika safu awe na utulivu na utaratibu ili asiwashawishi waswaliji.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/159)
  • Imechapishwa: 23/02/2026