Anaomba talaka kwa mume mwenye kansa

Swali: Mwanamke huyu alifunga ndoa na mume wake. Baada ya hapo ikadhihirika kuwa kuna chembechembe za kansa kwenye kiungo chake na hivyo akaanza kuongea na kuamini mkosi. Je, inafaa kwake kumuomba talaka? Je, huo ni mkosi unaozingatiwa kuuamini?

Jibu: Hapana, sio kuamini mkosi. Huko ni kwa sababu ya kuchukua tahadhari. Hapana vibaya ukiomba talaka. Ikithibiti kuwa yuko na kansa na mfano wake ni udhuru unaokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Huko ni katika kujitenga mbali na khatari.

Muulizaji: Je, amejitibisha na yuko vizuri?

Ibn Baaz: Ahimidiwe Allaah kama yuko vizuri.  

Muulizaji: Lakini bado anamwomba talaka?

Ibn Baaz: Hapana, haitakiwi kwake kumuomba.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24616/ما-يحل-لمن-اكتشفت-مرضا-بزوجها-بعد-العقد
  • Imechapishwa: 14/11/2024