Anakufuru mwanamke anayechukia mume wake kuongeza mke?

Swali: Je, kule mke kuchukia mume wake kuongeza mwanamke wa pili kunaingia katika kuyachukia yale aliyoteremsha Allaah? Kwani jambo hili pia limeteremshwa na Allaah.

Jibu: Hapana. Haya ni machukizo ya kimoyo/kimaumbile na sio kuchukia yale aliyoteremsha Allaah. Haina maana kwamba anachukia yale aliyoteremsha Allaah. Ikiwa atachukia yale aliyoteremsha Allaah anakufuru. Lakini si kwamba anachukia yale aliyoteremsha Allaah. Lakini ni kwamba anachukia madhara. Ni kwa sababu ya wivu. Hili ni jambo liko moyoni na wala haadhibiwi. Ni lazima kwake kufanya subira na aishinde nafsi yake. Ama kusema kwamba ni ukafiri sivyo. Kwa sababu haina maana kwamba mwanamke huyu anayachukia yale aliyoteremsha Allaah, hachukii ukewenza na wala hapingani nayo. Anachukia madhara na anachelea juu yake. Huu ni woga wa kimaumbile. Ni machukizo ya kimoyo. Haiathiri – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Naaqidh-il-Islaam http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/433/433.mp3
  • Imechapishwa: 23/11/2018