Anakufuru anayetamka neno la kufuru bila kuliamini ndani ya moyo wake?

Swali: Mtu anakufuru iwapo atasema neno alilolitaja kwa ulimi wake pasi na kuliamini moyoni mwake anakufuru?

Jibu: Ndio, akilisema hali ya kucheka kwa mfano akasema kuwa Muhammad ni mwongo au ni mfanya mchezo. Anakufuru haijalishi kitu hata kama hakuyaamini. Kwa mfano akasema kuwa Allaah hayuko juu ya mbingu japokuwa atafanya mchezo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 99
  • Imechapishwa: 26/07/2019