Swali: Ni ipi tafsiri ya maneno Yake Allaah:

يَمْحُو اللَّـهُ مَا يَشَاءُ وَيُثْبِتُ ۖ وَعِندَهُ أُمُّ الْكِتَابِ

“Allaah anafuta yale ayatakayo na anathibitisha na Kwake ndiko kuna Mama wa Kitabu.”[1]

Je, inakusudiwa kwamba anafuta yaliyomo ndani ya Qur-aan au kwenye Ubao uliohifadhiwa?

Jibu: Maana yake ni kwamba Allaah hufuta ayatakayo katika yale aliyoyaweka katika Shari´ah. Anafuta baadhi ya maandiko, kama ilivyotokea kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) alifuta baadhi ya hukumu zilizokuwa Makkah, na kisha Madiynah zikawa tofauti. Mfano ni suala la Qiblah ambapo mwanzoni walikuwa wakielekea Yerusalemu, kisha hukumu hiyo ikafutwa na wakaelekea Ka´bah. Vivyo hivyo yako mambo mengine yaliyotajwa kuwa yamefutwa. Kwa hiyo Allaah hufuta akitakacho. Kadhalika kuna mambo ambayo Yeye (Subhaanah) ameyaning´iniza yanapopatikana ndio hutokea na yasiyopatikana hayatokei. Allaah anafuta ayatakayo na kuyaweka ayatakayo kwa mujibu wa vile ilivyotangulia katika ujuzi Wake na makadirio Yake yaliyotangulia; mambo yote yanarejea Kwake na wala kubadiliki wala kugeuzwa kitu.

[1] 13:39

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31009/ما-تفسير-قوله-تعالى-يمحو-الله-ما-يشاء-ويثبت
  • Imechapishwa: 21/09/2025