Anafunga ili Allaah amtatulie mahitaji yake

Swali: Kuna mwanamke anapotaka Allaah amkidhie mahitaji yake basi hufunga. Ni ipi namna ya swawm hii?

Jibu: Kufunga kwa ajili ya kutatuliwa mahitaji ni Bid´ah na haina msingi. Hakika si venginevyo mtu anapaswa kujikurubisha kwa Allaah kwa aina mbalimbali za ´ibaadah zinazopendeza kwa ajili ya kumtii Allaah, kutafuta thawabu Zake hali ya kumtakasia nia Allaah pekee na si kwa ajili ya malengo ya kidunia. Miongoni mwa mambo yaliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwamba miongoni mwa wale ambao hazirudishwi nyuma du´aa zao ni pamoja vilevile na mfungaji mpaka atakapofungua na kwamba mfungaji anayo du´aa isiyorudishwa nyuma wakati wa kufungua kwake.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (09/292) nr. (20834)
  • Imechapishwa: 10/05/2022