Swali: Yule ambaye anadaiwa kulipa siku mbili za Ramadhaan na anataka kuzifunga siku ya tisa na ya kumi – je, zitamtosheleza kwa kulipa deni na pia kwa siku ya ´Aashuuraa´?
Jibu: Hapana shaka kwamba kulipa funga ya wajibu ni muhimu zaidi kuliko funga za kujitolea. Ikiwa mtu anadaiwa siku za Ramadhaan, siku za nadhiri au kafara, basi hizo ndizo za kipaumbele kuliko sunnah. Akifunga siku ya ´Arafah au siku ya ´Aashuuraa´ kwa nia ya kulipa deni, basi hakuna neno. Tunatumaini kwamba Allaah atamkusanyia kheri mbili na thawabu mbili; ikiwa hakumzuia kufunga ´Aashuuraa´ isipokuwa kulipa siku alizodaiwa na siku zilizo juu yake. Kwa hiyo anatarajiwa kupata fadhilah ya hili na lile.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2590/حكم-صيام-عاشوراء-قضاء
- Imechapishwa: 28/03/2026
Swali: Yule ambaye anadaiwa kulipa siku mbili za Ramadhaan na anataka kuzifunga siku ya tisa na ya kumi – je, zitamtosheleza kwa kulipa deni na pia kwa siku ya ´Aashuuraa´?
Jibu: Hapana shaka kwamba kulipa funga ya wajibu ni muhimu zaidi kuliko funga za kujitolea. Ikiwa mtu anadaiwa siku za Ramadhaan, siku za nadhiri au kafara, basi hizo ndizo za kipaumbele kuliko sunnah. Akifunga siku ya ´Arafah au siku ya ´Aashuuraa´ kwa nia ya kulipa deni, basi hakuna neno. Tunatumaini kwamba Allaah atamkusanyia kheri mbili na thawabu mbili; ikiwa hakumzuia kufunga ´Aashuuraa´ isipokuwa kulipa siku alizodaiwa na siku zilizo juu yake. Kwa hiyo anatarajiwa kupata fadhilah ya hili na lile.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2590/حكم-صيام-عاشوراء-قضاء
Imechapishwa: 28/03/2026
https://firqatunnajia.com/anafunga-deni-la-ramadhaan-siku-ya-aashuuraa-na-arafah/