Swali: Ipi hukumu ya mwenye kufunga na haswali au anaswali Dhuhr na ´Aswr mwisho wa ´Aswr na hii ndio ada yake?

Jibu: Anayefunga na haswali hana swawm. Kwakuwa anayeacha swalah hakubaliwi kutoka kwake matendo mengine mpaka ahifadhi swalah zake. Swalah ndio imesisitizwa zaidi kuliko swawm. Swalah ndio nguzo ya pili. Na swawm ni nguzo ya nne. Swalah ndio msingi wa matendo.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/allmohadrat?page=4
  • Imechapishwa: 15/05/2018