Swali: Mimi daima huapa kuwa nitafanya jambo fulani na silifanyi na huapa kwamba nitamlipia ndugu yangu kwenye mgahawa ambapo yeye akalipa kabla yangu. Nifanye nini?

Jibu: Ikiwa umeteleza kuapa bila kukusudia, hakuna kinachokulazimu. Ni kiapo kisichokuwa na maana. Lakini kama umekusudia kuapa na baadaye ukavunja kiapo chako, au yule mwingine akafanya kile ambacho umekiapia, unalazimika kutoa kafara kwa ajili ya jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 28/06/2024