Swali: Ni yepi maoni yenye nguvu zaidi kuhusu suala la maji? Tafadhali tufafanulieni. Ni ipi tiba ya wasiwasi unaopitiliza katika twahara? Nina rafiki yangu anayesumbuliwa sana na wasiwasi huu, kiasi kwamba wakati mwingine huacha baadhi ya nguo zake kwa sababu ya khofu ya kufikiwa na matone ya maji yanayomwagika bafuni wakati wa kutawadha. Mwishowe aliacha kuswali, ambapo nikamnasihi mpaka akaanza kuswali tena. Hata hivyo ameniomba nimwelekeze tiba ya wasiwasi huu.
Jibu: Mosi ni kwamba msingi wa hukumu ya maji ni kuwa ni twahara. Ikiwa rangi, ladha au harufu yake itabadilika kwa sababu ya najisi, basi maji hayo ni najisi, ni mamoja yawe machache au mengi. Lakini ikiwa najisi haikuyabadilisha, basi ni maji yenye kutwaharisha. Hata hivyo ikiwa ni machache sana, basi ni vizuri kutoyatumia kwa twahara kwa ajili ya kuchukua tahadhari, kujiepusha na tofauti za wanazuoni na kutekeleza Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mbwa akilamba chombo cha mmoja wenu, basi akimwage… ”
Pili ni kwamba tiba ya wasiwasi huu ni kumtaja Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa wingi na kumuomba Allaah ampe afya na amkinge na hali hiyo na kutokubali kutawaliwa na wasiwasi. Ni wajibu kwake kuupuuza. Kwa mfano akifanya twahara ndogo au twahara kubwa, kisha akapatwa na wasiwasi kwamba hakuiosha kichwa chake, basi asiupe umuhimu wasiwasi huo. Bali ajenge juu ya kwamba amekiosha. Vivyo hivyo katika matendo yake mengine anatakiwa kukataa kuitikia wasiwasi huo, kwa sababu unatoka kwa Shaytwaan. Pia anatakiwa kuzidisha kuomba kinga kwa Allaah dhidi ya Shaytwaan, kwa sababu yeye ndiye mwenye kutia wasiwasi vifuani mwa watu.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/225-226)
- Imechapishwa: 09/11/2026

Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/225-226)
Imechapishwa: 09/11/2026
https://firqatunnajia.com/ana-wasiwasi-sana-katika-twahara-mpaka-amefikia-kuacha-swalah/