64. Fidia ambayo ni lazima kuifanya kwa mpangilio

2 – Ni ile ambayo haina chaguo, bali inafuata mpangilio maalum. Naye ni mwenye kufanya Hajj ya Tamattu´, ambaye ni wajibu kwake kuchinja mbuzi mmoja. Ikiwa hatapata, basi atafunga siku tatu akiwa katika Hajj na siku saba atakaporudi.

Fidia ya kufanya tendo la ndoa ni kuchinja ng´ombe au ngamia. Ikiwa hatapata, basi atafunga kama anavyofunga mwenye kufanya Hajj ya Tamattu´.

Hukumu hiyohiyo inahusu fidia ya kukosa Hajj.

Yule mwenye kuzuiwa kuendelea na Hajj au ´Umrah ni wajibu kwake kuchinja mnyama wa fidia. Ikiwa hatapata, basi atafunga siku kumi.

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 46
  • Imechapishwa: 09/11/2026