Swali: Hadiyth:

“Badilisheni mvi.”

Je, ni kwa njia ya ulazima?

Jibu: Msingi ya amri ni kuwa ni wajibu, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kisa cha Abu Bakr as-Swiddiyq:

“Badilisheni mvi hizi na jiepusheni na rangi nyeusi.”

Lakini inadhihiri kutokana na kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baadhi ya Maswahabah kuwa jambo hilo si la wajibu, bali ni Sunnah iliyosisitizwa kubadilisha rangi ya mvi. Kwa sababu imekuja dalili kuwa katika ndevu zake zilionekana nywele chache nyeupe ambazo hakuzibadilisha. Vilevile Maswahabah walikuwa wakati mwingine wanakaa masiku kadhaa bila kubadilisha rangi ya mvi, kisha wakazibadilisha baadaye. Kwa hivyo kilicho karibu zaidi – Allaah ndiye Mjuzi zaidi – ni kuwa ni Sunnah iliyosisitizwa.

Swali: Je, Hadiyth hii ni Swahiyh?

Jibu: Haina tatizo. Cheni yake ya wapokezi ni nzuri. Haina neno.

Swali: Je, kuna yeyote anabaguliwa kutolewa katika hukumu hii kama mfano wa wanaopambana jihaad katika njia ya Allaah?

Jibu: Sijui kuhusu aina yoyote ya kubaguliwa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31631/هل-الامر-في-حديث-غيروا-الشيب-للوجوب
  • Imechapishwa: 21/12/2025