Swali: Mtoto wangu aliwahi kuugua akiwa mdogo, ugonjwa mkali sana. Nikasema kwamba ikiwa Allaah atamponya, basi nitafunga mwezi wa Rajab kila mwaka. Sasa hivi sijawahi kufunga hata mara moja, kwa sababu kila mwaka huwa mjamzito au ninanyonyesha. Huu unakamilisha takriban miaka tisa tangu natoa nadhiri hiyo. Mimi siwezi kufunga na nadhiri yenyewe si sahihi. Nifanye nini?
Jibu: Hio ni nadhiri ya kuchukiza. Kumuahidi Allaah kufunga mwezi wa Rajab kila mwaka ni jambo linalochukiza. Kwa hiyo anachotakiwa ni kutoa kafara ya kiapo na kufanya hivo inatosha. Hii ni kwa sababu kufunga Rajab kama ´ibaadah maalum ni jambo linalochukiza. Nadhiri yenyewe pia ni ya kuchukiza. Basi inamtosha kutoa kafara ya kiapo: awalishe masikini kumi, kila mmoja nusu pishi ya chakula kinacholiwa katika mji wake au kuwavisha nguo. Hilo linatosha na hana wajibu wa kufunga.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1097/نذرت-صيام-شهر-رجب-من-كل-عام
- Imechapishwa: 15/12/2025
Swali: Mtoto wangu aliwahi kuugua akiwa mdogo, ugonjwa mkali sana. Nikasema kwamba ikiwa Allaah atamponya, basi nitafunga mwezi wa Rajab kila mwaka. Sasa hivi sijawahi kufunga hata mara moja, kwa sababu kila mwaka huwa mjamzito au ninanyonyesha. Huu unakamilisha takriban miaka tisa tangu natoa nadhiri hiyo. Mimi siwezi kufunga na nadhiri yenyewe si sahihi. Nifanye nini?
Jibu: Hio ni nadhiri ya kuchukiza. Kumuahidi Allaah kufunga mwezi wa Rajab kila mwaka ni jambo linalochukiza. Kwa hiyo anachotakiwa ni kutoa kafara ya kiapo na kufanya hivo inatosha. Hii ni kwa sababu kufunga Rajab kama ´ibaadah maalum ni jambo linalochukiza. Nadhiri yenyewe pia ni ya kuchukiza. Basi inamtosha kutoa kafara ya kiapo: awalishe masikini kumi, kila mmoja nusu pishi ya chakula kinacholiwa katika mji wake au kuwavisha nguo. Hilo linatosha na hana wajibu wa kufunga.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1097/نذرت-صيام-شهر-رجب-من-كل-عام
Imechapishwa: 15/12/2025
https://firqatunnajia.com/ameweka-nadhiri-ya-kufunga-rajab-kila-mwaka/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket