Ameweka nadhiri ya kufunga miezi miwili na sasa ni mgonjwa hawezi

Swali: Kuna mwanamke ni mtumzima ambaye alijiwekea nadhiri mwenyewe ya kafara kikali ya kufunga miezi miwili mfululizo au kuacha mtumwa huru. Hivi sasa ni fakiri na ni mgonjwa wa maradhi ya sukari. Alianza kufunga lakini hakuweza kumaliza. Ni kipi kinachomlazimu?

Jibu: Dhahiri ni kwamba ni wajibu kwake kuwalisha masikini sitini. Kwa sababu kafara kali ni ima kuacha mtumwa huyu, asipopata afunge miezi miwili mfululizo, asipoweza basi awalishe masikini sitini. Ni wajibu kwake kuwalisha masikini sitini.

Napenda kuwakumbusha kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza nadhiri na akaeleza kwamba hairudishi aliyopanga Allaah na kwamba haileti kheri. Sikiza maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haina manufaa ya kidini wala ya kimakadirio.

Baadhi ya watu wanapopatwa na ugonjwa na wakaweka nadhiri, wanafikiri kwamba wakiweka nadhiri kwamba Allaah ndipo atawaponya. Hili ni kosa. Ikiwa Allaah anataka kukuponya basi atafanya hivo pasi na kuweka nadhiri. Na ikiwa Allaah hataki kufanya hivo basi haitofaa nadhiri hiyo…

Mtii Allaah pasi na kuweka nadhiri. Kwani kuweka nadhiri imechukizwa. Bali wapo wanachuoni ambao wameiharamisha. Kwa ajili hii utawaona wengi ambao wanaweka nadhiri baadaye kujita sana na kuanza kuwauliza watu wafanye nini na kwamba wawafanyie wepesi. Baadhi ya wengine Allaah anawapa kile walichomuwekea Allaah nadhiri, lakini hawatimizi ahadi zao. Jambo hili khatari yake ni kubwa. Khatari yake ni:

فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِي قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُ بِمَا أَخْلَفُوا اللَّـهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ

“Basi akawaadhibu kwa unafiki katika nyoyo zao mpaka siku watakayokutana Naye kutokana na yale walivyomkhalifu kwao Allaah kwa waliyomuahidi na kutokana na yale waliyokuwa wakikadhibisha.”[1]

Huenda Allaah akaweka unafiki kwenye moyo wa mtu huyu mpaka pale atapofariki. Allaah atulinde sote kutokamana na hilo.

[1] 09:77

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (52) http://binothaimeen.net/content/1174
  • Imechapishwa: 15/06/2020