Amevaa soksi ya mguu wa kulia kabla kuosha mguu wa kushoto

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu ambaye ameosha mguu wake wa kulia, kisha akavaa soksi kabla ya kuosha mguu wake wa kushoto?

Jibu: Haijuzu kupangusa juu ya soksi hizo, kwa sababu uliingiza soksi ya mguu wa kwanza kabla ya kukamilisha twahara.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/247)
  • Imechapishwa: 06/11/2026