Ametawadha kabla ya kutamba

Swali: Mtu aliosha mikono yake, uso wake, mikono yake mpaka kwenye viwiko na miguu yake, kwa maana akatawadha kabla ya kutamba. Baada ya kutawadha akatamba. Ni ipi hukumu?

Jibu: Ikiwa hali ni kama ulivyoeleza, wudhuu´ wake si sahihi, kwa sababu miongoni mwa masharti ya usahihi wa wudhuu´ ni kutanguliwa na kujisafisha kwa maji au kwa mawe baada ya kutoka mkojo au kinyesi, kwa mujibu wa maoni yenye nguvu zaidi ya wanazuoni.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/233-234)
  • Imechapishwa: 06/11/2026