Muhammad bin Abiy Haatim amesema:

“al-Bukhaariy amesema: “Ishaaq bin Ibraahiym aliulizwa juu ya ambaye ametaliki kimakosa. Akanyamza kwa muda mrefu akifikiri, swali ameshaulizwa. Mimi nikasema: “Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah ameusamehe Ummah wangu yale yanayonong´onezwa na nafsi zao wenyewe muda wa kuwa hawajayafanya wala kuyazungumza.”[1]

Bi maana ni lazima kufanya mambo haya matatu; kitendo na moyo au maneno na moyo. Mtu huyu hakuonelea hivo ndani ya moyo wake. Ishaaq akasema: “Umenitia nguvu” na akatoa fatwa hiyo baada yangu.

[1] al-Bukhaariy (5269) na Muslim (127).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/414)
  • Imechapishwa: 20/11/2020