Ameswali bila ya kutawadha baada kula nyama ya ngamia

Swali: Kuna mtu amekula nyama ya ngamia na hakutawadha hali ya kuwa anajua hukumu na maji yapo. Je, swalah yake inabatilika?

Jibu: Ndio, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kutawadha baada ya kula nyama ya ngamia:

”Tawadheni kutokana na nyama ya ngamia na msitawadhe kutokana na nyama ya kondoo.”

Vilevile aliulizwa: ”Ee Mtume wa Allaah. Je, tutawadhe kutokana na nyama ya ngamia?” Akasema: ”Ndio.”

Basi yule anayeswali na hali ya kuwa amekula nyama ya ngamia bila ya kutawadha, atarudia swalah ikiwa hakutawadha. Hivi ndivo ilivyowekwa katika Shari´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30969/ما-حكم-صلاة-من-لم-يتوضا-من-لحم-البعير
  • Imechapishwa: 18/09/2025