Amesoma al-Faatihah katika Tashahhud kwa kusahau

Swali: Kuna mtu amesoma al-Faatihah katika Tashahhud kwa kusahau. Je, arudi swalah yake?

Jibu: Asiirudi swalah yake akisoma al-Faatihah katika Tashahhud kwa kusahau. Lakini hata hivyo ni wajibu kwake kusoma Tashahhud. Kwa sababu Tashahhud ya mwisho inayofuatiwa na salamu ni nguzo. Kuhusu Tashahhud ya kwanza au ya kati kati ni wajibu miongoni mwa mambo ya wajibu ya swalah. Itambulike kuwa imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Tanabahini! Mimi nimekatazwa kusoma Qur-aan hali ya kuwa nimerukuu au nimesujudu.”

Hivyo haijuzu kwa mwenye kuswali kusoma Qur-aan hali ya kuwa amerukuu au amesujudu. Pamoja na hivyo ni sawa iwapo atasoma du´aa iliyo na Qur-aan. Ama kusoma Qur-aan hali ya kuwa amerukuu au amesujudu ni kitendo cha haramu kwake. Baadhi ya wanachuoni wanaonelea kuwa mwenye kusoma Qur-aan hali ya kuwa ameruku au amesujudu swalah yake inabatilika kwa kuwa amekatazwa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (07)
  • Imechapishwa: 01/05/2020