Ameshindwa kulipa kwa sababu Ramadhaan ya kwanza mimba na ya pili amezaa

Swali: Kuna mwanamke alikula siku tano za Ramadhaan na hakuwahi kulipa mpaka akashika mimba nyingine. Alipotaka kulipa hakuweza. Amekadiria kuwa atazaa wakati wa Ramadhaan na kwamba hawezi kufunga pia. Afanye nini? Je, alipe mwezi wa Ramadhaan hii na zile siku tano za mwaka ule au alishe juu ya zile siku tano na alipe Ramadhaan ya mwaka huu?

Jibu: Mambo yakiwa kama alivyosema alipe zile siku tano na alipe Ramadhaan ya mwaka huu na wala halazimiki kutoa kafara.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/343)
  • Imechapishwa: 18/06/2017