Swali: Maamuma amechelewa kusoma al-Faatihah kwa sababu ya kusahau kisha imamu akarukuu.

Jibu: Arukuu na hakuna kitu kinachomlazimu. al-Faatihah inamdondokea kwa kusahau na inamdondokea kwa kutokujua.

Swali: Nakusudia kuwa imamu amerukuu kabla ya kuimaliza?

Jibu: Arukuu na wala asisubiri. Arukuu na aikate.

Swali: Mtu anaweza kusema alete Rak´ah nyingine.

Jibu: Hapana, aikate na arukuu pamoja na imamu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21647/حكم-من-سها-عن-الفاتحة-حتى-ركع-الامام
  • Imechapishwa: 08/09/2022