Swali: Tulikwenda kupiga vijiwe siku ya pili ya siku za Tashriyq, lakini kwa sababu ya msongamano mkubwa hatukuweza kuyaona mawe. Hivyo mimi na baba yangu tulikuwa tukirusha mawe bila kujua kama yamelenga nguzo au hapana, ingawa dhana kubwa ni kwamba hayakufika. Je, chochote kinachotuwajibikia? Kwa kuwa nilimuuliza Shaykh ninayemuamini katika elimu na uadilifu wake, akasema kwamba tunawajibika kuchinja, lakini hakunieleza lini, vipi na wapi. Nimerudia kuuliza kwenu ili kupata ufafanuzi zaidi tu.
Jibu: Ikiwa dhana yenu kubwa ni kwamba mawe hayakufika kwenye nguzo, kama ulivyosema, basi ni juu yenu kuchinja, kama alivyowapa fatwa yule aliyefanya hivo. Ikiwa unaona kwa dhana kubwa kuwa mawe hayakufika kwenye nguzo na hamkujua kama yalifika, basi mnatakiwa kutoa fidia ya kuchinja mnyama. Wewe unatakiwa kuchinja mnyama mmoja na baba yako pia mnyama mmoja, kwa sababu kupiga mawe ni wajibu. Kwa hiyo ikiwa haikuwa na nguvu dhana yako kuwa yamefika na wala hamkujua kuwa yamefika, basi mchinje wanyama kwa nia ya fidia ya hijjah ile mliyofanya.¨Wewe una mmoja na baba yako ana mmoja. Fatwa uliyopewa ni sahihi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3287/حكم-من-لم-يتيقن-وصول-الحصى-في-حوض-الجمرات
- Imechapishwa: 07/08/2026
Swali: Tulikwenda kupiga vijiwe siku ya pili ya siku za Tashriyq, lakini kwa sababu ya msongamano mkubwa hatukuweza kuyaona mawe. Hivyo mimi na baba yangu tulikuwa tukirusha mawe bila kujua kama yamelenga nguzo au hapana, ingawa dhana kubwa ni kwamba hayakufika. Je, chochote kinachotuwajibikia? Kwa kuwa nilimuuliza Shaykh ninayemuamini katika elimu na uadilifu wake, akasema kwamba tunawajibika kuchinja, lakini hakunieleza lini, vipi na wapi. Nimerudia kuuliza kwenu ili kupata ufafanuzi zaidi tu.
Jibu: Ikiwa dhana yenu kubwa ni kwamba mawe hayakufika kwenye nguzo, kama ulivyosema, basi ni juu yenu kuchinja, kama alivyowapa fatwa yule aliyefanya hivo. Ikiwa unaona kwa dhana kubwa kuwa mawe hayakufika kwenye nguzo na hamkujua kama yalifika, basi mnatakiwa kutoa fidia ya kuchinja mnyama. Wewe unatakiwa kuchinja mnyama mmoja na baba yako pia mnyama mmoja, kwa sababu kupiga mawe ni wajibu. Kwa hiyo ikiwa haikuwa na nguvu dhana yako kuwa yamefika na wala hamkujua kuwa yamefika, basi mchinje wanyama kwa nia ya fidia ya hijjah ile mliyofanya.¨Wewe una mmoja na baba yako ana mmoja. Fatwa uliyopewa ni sahihi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3287/حكم-من-لم-يتيقن-وصول-الحصى-في-حوض-الجمرات
Imechapishwa: 07/08/2026
https://firqatunnajia.com/amerusha-vijiwe-lakini-anadhani-kuwa-hayakulenga-nguzo/