Amepita kituo kwa sababu ya ujinga

Swali: Kuna mtu alitembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Madiynah na akanuia kufanya ´Umrah. Hajui kituo maalum cha watu wa Madiynah ambapo akaenda Makkah na alipokuwa njia akapata kujua kuwa ataingia kwenye Ihraam kilomita 70-80 kabla ya Makkah. Kabla ya kuingia akajuzwa kwamba ataingia kwenye Ihraam kutokea Tan´iym. Ni ipi hukumu ya ´Umrah yake?

Jibu: ´Umrah yake ni sahihi. Lakini ni lazima atoe fidia kwa kuacha kwake Ihraam kutoka kwenye kituo cha Madiynah. Atalazimika kutoka fidia, kwa sababu ameacha jambo la wajibu miongoni mwa mambo ya wajibu ya Hajj.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (22) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdatul-26-3-1435.mp3
  • Imechapishwa: 25/03/2020