Ameokota kilichopotea kisha kikamuharibikia

Swali: Ikiwa mtu atachukua kitu kilichopotea kwa nia ya kukitangaza kisha kikaharibika – je, anapaswa kukilipa?

Jibu: Ikiwa amekitelekeza kwa uzembe, basi anapaswa kukilipa. Lakini ikiwa hakufanya uzembe wala hakuvuka mpaka wake, basi hawajibiki.

Swali: Ikiwa kitu kilichopotea ni chakula ndani ya msikiti wa Haram na anakhofu kikaharibika?

Jibu: Anapaswa kukiuza na kuhifadhi thamani yake. Aweke kumbukumbu za sifa za kitu hicho, kisha akiuze na kuhifadhi thamani yake ili imfikie mmiliki wake. Hii pia inajumuisha mavazi au vitu vingine vinavyoweza kuharibika.

Swali: Je, mtu analazimika kuchukua kitu kilichopotea ikiwa ana khofu kwamba kitaharibika?

Jibu: Hapana, haimlazimu.

Swali: Hata kama anaogopa kitaharibika?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakusema kichukuliwe, bali alieleza tu majukumu ya mtu ikiwa amekichukua. Kwa hivyo si lazima mtu ajilazimishe kuchukua kitu kilichopotea.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25424/حكم-من-التقط-لقطة-بنية-التعريف-ثم-تلفت-عنده
  • Imechapishwa: 24/03/2025