Swali: Baba yangu alimkanyaga mtoto mwenye umri wa takriban miaka miwili. Sababu ya tukio ni kwamba baba yangu alikuwa na gari na lilikuwa limesimama. Kabla hajaingia ndani ya gari alitazama chini pande zote na hakuona mtu. Akaingia kwenye gari. Katika wakati huo mmoja wa ndugu wa mtoto akamchukua mtoto na kumuweka chini ya gurudumu la mbele bila baba yangu kujua. Alipoanza kuondoka akamkanyaga mtoto. Je, inampasa kufunga miezi miwili au hapana?
Jibu: Kama ilivyokuja katika kafara, inampasa kufunga miezi miwili kama anaweza. Kama ataweza huru kuachia mtumwa, mwenye gari aliyemkanyaga, kwa sababu yeye ndiye aliyetekeleza kitendo cha kuua. Basi juu yake ipo fidia ya damu na juu yake ipo kafara.
Kafara ni kuachia huru mtumwa mwenye imani ikiwa itawezekana. Ikiwa haitowezekana basi juu yake ni kufunga miezi miwili mfululizo, kama Allaah alivyobainisha katika Kitabu Chake kitukufu katika Suurah ”an-Nisaa”. Yeye ndiye aliyekanyaga na yeye ndiye muuaji, kwa sababu yule aliyemuweka mtoto hapo hakuwa na kusudio la kumuua. Lakini kama, kama alivosema Shaykh, lau angelikuwa mtu akamchukua mtu mwingine na kumtupa mbele ya gari ili mwenye gari amkanyage bila kujua, hapo angekuwa ndiye muuaji yule aliyemtupa mbele ya gari. Lakini katika hali hii, mtoto aliwekwa hapo pengine kwa ajili ya kivuli au sababu nyingine. Tunasema: Allaah amekadiria mauti yake kupitia gari hii. Basi aliyemkanyaga ndiye anayetakiwa kutoa fidia ya damu na kafara vyote kwa pamoja.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/990/حكم-من-قتل-طفلا-بسيارته-خطا
- Imechapishwa: 06/01/2026
Swali: Baba yangu alimkanyaga mtoto mwenye umri wa takriban miaka miwili. Sababu ya tukio ni kwamba baba yangu alikuwa na gari na lilikuwa limesimama. Kabla hajaingia ndani ya gari alitazama chini pande zote na hakuona mtu. Akaingia kwenye gari. Katika wakati huo mmoja wa ndugu wa mtoto akamchukua mtoto na kumuweka chini ya gurudumu la mbele bila baba yangu kujua. Alipoanza kuondoka akamkanyaga mtoto. Je, inampasa kufunga miezi miwili au hapana?
Jibu: Kama ilivyokuja katika kafara, inampasa kufunga miezi miwili kama anaweza. Kama ataweza huru kuachia mtumwa, mwenye gari aliyemkanyaga, kwa sababu yeye ndiye aliyetekeleza kitendo cha kuua. Basi juu yake ipo fidia ya damu na juu yake ipo kafara.
Kafara ni kuachia huru mtumwa mwenye imani ikiwa itawezekana. Ikiwa haitowezekana basi juu yake ni kufunga miezi miwili mfululizo, kama Allaah alivyobainisha katika Kitabu Chake kitukufu katika Suurah ”an-Nisaa”. Yeye ndiye aliyekanyaga na yeye ndiye muuaji, kwa sababu yule aliyemuweka mtoto hapo hakuwa na kusudio la kumuua. Lakini kama, kama alivosema Shaykh, lau angelikuwa mtu akamchukua mtu mwingine na kumtupa mbele ya gari ili mwenye gari amkanyage bila kujua, hapo angekuwa ndiye muuaji yule aliyemtupa mbele ya gari. Lakini katika hali hii, mtoto aliwekwa hapo pengine kwa ajili ya kivuli au sababu nyingine. Tunasema: Allaah amekadiria mauti yake kupitia gari hii. Basi aliyemkanyaga ndiye anayetakiwa kutoa fidia ya damu na kafara vyote kwa pamoja.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/990/حكم-من-قتل-طفلا-بسيارته-خطا
Imechapishwa: 06/01/2026
https://firqatunnajia.com/amemuua-mtoto-wake-kwa-gari-yake-kimakosa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket