Swali: Mwanaume alimuoa mwanamke ambaye alifanya naye uasherati kabla ya ndoa. Haikuwa kwa matakwa yake, bali limetokea kwa bahati mbaya kwa shaytwaan kuingia kati yao. Kwa sababu ya kuogopa fedheha na aibu alimuoa na akazaa naye watoto, lakini dhambi ni ile inayomkera mtu ndani ya moyo wake na ukachukia watu wasije kuijua mashaka yake kwake kila mara ndiyo yanayomfanya kweli aone yaliyopita kila mara mbele ya macho yake na yanamfanya amshuku mwanamke huyo. Anaona kana kwamba kile alimpa yeye kabla ya ndoa atampa mwingine baada ya yeye kumuoa. Matokeo yake akamwacha na akapata faraja ya nafsi kweli baada ya kufanya hivo. Je, ana dhambi kwa kufanya hivo? Ni ipi hali ya watoto wake katika mfano wa hali hii? Je, katika hilo kuna jambo upande wa kidini? Je, ana haki ya kulea watoto wake au kuwarudisha kutokana na kuwa ndiye aliyemjaribu hapo mwanzo kabla ya ndoa na akamvuta kufanya uasherati kwa sababu huenda malezi ya mwanamke huyo yasiwe ya Kiislamu? Kwa kuzingatia pia kwamba kumuoa kwake hapo mwanzo ilikuwa kwa kuogopa adhabu ya Allaah (´Azza wa Jall). Aidha ijulikane kwamba nwanamke huyo alikuwa ameshaolewa baada ya yeye kumuoa.
Jibu: Ikiwa kumuoa kwake kulikuwa baada ya tawbah, basi hakuna ubaya katika hilo. Ikiwa mwanamke huyo alionyesha kutubu na kujutia na yeye mwanaume vivyo hivyo, basi hakuna ubaya kumuoa kwa ajili ya kumsitiri na kuficha kilichotokea. Yeyote atakayemsitiri muislamu basi Allaah atamsitiri duniani na Aakhirah. Lakini ikiwa alimuoa kwa ajili ya kumsitiri tu, kwa sababu ya mashinikizo ya baba yake au mama yake au mengineyo, naye mwanamke huyo yuko katika hali yake ileile – hakuonyesha kutubu – basi haijuzu ndoa hiyo wala haifai. Ni lazima kwa mwanamke huyo kutubu kutokana na hilo. Umefanya vizuri katika kumtaliki ikiwa dhahiri yake ni kutokuwa na uongofu. Watoto wako wanahesabiwa wako kwa ajili ya shubuha ya ndoa. Watoto wako wanahesabiwa wako kwa ajili ya shubuha ya ndoa, hata kama ndoa hiyo ni batili ikiwa hakutubia kutokana na kitendo chake kiovo. Umefanya vizuri kama ilivyotangulia katika kumtaliki ikiwa hali yake ni mbaya. Ama ikiwa alikwishatubia na akaonyesha majuto na wewe pia hivyohivyo na mlikifanya hilo kwa kusitiri na kuondoa shari, basi nyinyi mko katika kheri wala hakuna dhambi juu yenu – Allaah akitaka. Lakini kwa kuwa bado haijaonekana tawbah kutoka kwake na unaogopa kuwa atafanya na mwingine kama alivyofanya na wewe na kwa ajili hiyo ukamtaliki, basi umefanya vizuri katika hilo na watoto ni watoto wako.
Kuhusu kwamba wanabaki kwake au kuhamishiwa kwako hilo ni la mahakamani, si la kwetu sisi. Lakini ikiwa mtapatana baina yenu – pamoja na baba yake na jamaa zake – kuwa wawe kwako kwa kuogopa juu ya watoto wako, hilo halina ubaya. Ikiwa amenyooka sawasawa na hali yake imekuwa nzuri, basi hakuna ubaya kwa watoto kubaki naye. Ikiwa hali yake imekuwa nzuri, lakini wewe kwa sababu ya shaka na wasiwasi ukamtaliki, basi hapana vibaya kwa watoto kubaki naye kwa kuwa hali yake imekuwa nzuri. Ama ikiwa unamdhania vibaya na huoni kwamba hali yake imekuwa nzuri, basi fanya unaloweza katika njia za Kishari´ah na mahakama ili kuhamisha watoto kwako au kwa kupitia watu wema wafanye suluhu kati yenu mpaka yeye na jamaa zake wakubali kukupa watoto wako. Ikiwa hilo halitawezekana basi uende mahakamani bila ya kueleza jambo la uzinzi. Lakini dai watoto wako na sema kwamba unakhofia juu yao.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29384/حكم-من-تزوج-من-زنا-بها-للستر-ثم-شك-بحالها-فطلقها
- Imechapishwa: 05/08/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29384/حكم-من-تزوج-من-زنا-بها-للستر-ثم-شك-بحالها-فطلقها
Imechapishwa: 05/08/2025
https://firqatunnajia.com/amemuoa-mwanamke-aliyemzini-kisha-baadaye-akamtaliki-kwa-kutomwamini/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket